ZANZIBAR GERMAN VOCATIONAL TRAINING PARTNERSHIP

VTAGERMANYlogobunners

Toggle Navigation
Open menu
  • NYUMBANI
  • KUHUSU SISI
    • Washirika wa Mradi
    • Wafuasi
    • Timu
    • KAMATI TENDAJI
  • MRADI
    • Shughuli za Awamu ya Kwanza
      • Mafunzo kwa Walimu
      • Ushirikiano na Sekta Binafsi
      • Kuboresha Sifa za Walimu
    • Shughuli za Awamu ya Pili
      • Chuo cha Walimu
      • Ushirikiano na Sekta Binafsi
      • Mfumo ya Dual Apprenticeship
  • NYARAKA ZA KIELEKTRONIKI
    • MAUDHUI YA KUFUNDISHIA
  • MEDIA
    • PICHA
    • VIDEO
    • MACHAPISHO
  • MAWASILIANO
    • Meneja wa Mradi
    • Mratibu wa Mradi
    • Mratibu wa Mradi Sekta Binafsi
    • Maoni

MAELEZO YA MRADI

GERMAN COOPERATION

Huu ni mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani wenye nia ya kuongeza ufanisi wa ndani katika vituo vya mafunzo ya amali na kuifanya elimu ya mafunzo ya amali iwe ya vitendo zaidi.

Mradi huu unalenga sana kwa vituo vya mafunzo ya amali vya serikali na vituo binafsi vya mafunzo ya amali vilivyosajiliwa na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali (MMA) Zanzibar. Shughuli zote za mradi huu zinazingatia athari za muda mrefu.

Kulingana na uhusiano wa muda mrefu uliopo baina ya miji miwili, mji mkongwe wa Zanzibar na Potsdam wa Ujerumani, mradi ulianzishwa na kuendelezwa kupitia lengo la kuwa na umoja na kuendelezwa kupitia lengo la kuwa na umoja na ni matunda ya majadiliano ya wajumbe kutoka miji hio miwili.

Malengo ya Mradi

Kuhakikisha kuwa na wahitimu wenye sifa katika mafunzo ya amali wana nafasi kubwa na matarajio bora ya kuajiriwa au kujiajiri.

Muda wa Mradi

Muda wa mradi huu una awamu mbili (2), awamu ya kwanza ilikuwa ya miaka mitatu (3) kutoka mwaka 2017 mpaka 2020 na awamu ya pili ya miaka mitatu (3) mingine kuanzia mwaka 2020 mpaka 2023. Kimsingi mradi huu unaendeshwa na meneja mradi anaeishi Zanzibar, mratibu wa mradi sekta ya umma (MMA) na mratibu mradi sekta binafsi (ZNCC).

Tafuta

Habari Zilizopita / Tupo Facebook

VTA GERMAN PARTNERSHIP

Back to Top

© 2021 ZANZIBAR GERMAN VOCATIONAL TRAINING PARTNERSHIP