50620480 2402469033157423 8711750447313977344 o

Partners

Mamlaka Ya Mafunzo Ya Amali Zanzibar (MMA)

 

Ni Mamlaka kamili ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali. Na imepewa wajibu wa :

  1. Kusimamia mafunzo ya amali kwa kuweka viwango vya mafunzo, kutathmini vituo vya mafunzo ya amali, kusajili vituo vya mafunzo ya amali, kutathmini uwezo na ujuzi wa walimu na wanafunzi.
  2. Kuratibu mafunzo ya amali kwa kufanya utafiti wa soko la ajira, kuandaa na kubuni mpango (mitaala, mitaala ya kozi za muda mrefu na kozi za muda mfupi ), kushughulika na mafunzo ya amali, kuimarisha uwezo na maendeleo ya ujuzi wa walimu na viongozi wa mafunzo ya amali.
  3. kuhakikisha uwepo wa fedha za kutosha katika uendeshaji wa mfumo wa mafunzo ya amali.
  4. kutoa mafunzo ya amali.
  5. Kuthibitisha vyeti vinavyotolewa vimesajiliwa na Vyuo vya Mafunzo ya Amali

 www.zvta.go.tz

 

Mamlaka ya Mafunzo ya Amali (AVT) Teltow - Ujerumani 

Ni mtoa huduma kiongozi wa mafunzo ya amali katika jiji la Berlin Brandenburg, Ujerumani. Zaidi ya wanafunzi 2000 wanapata mafunzo kila mwaka katika fani mbalimbali na viwango vya elimu tofauti.

www.avt-bildung.de

 

 

Co-Partners 

ZNCC

Jumuiya ya kitaifa ya wafanyabaishara, Zanzibar (ZNCC)

Ilianzishwa ili kuunganisha sauti za wanachama na kutoa huduma kuendana na  mahitaji yao. ZNCC ni kiungo baina ya wanachama wake na serikali pamoja na wadau wengine.

www.zncc.or.tz

 

KIST

Ni taasisi ys serikali chini ya wizara ya elimu na mafunzo ya amali. Taasisi iliyokabidhiwa jukumu la kuhifadhi, kuimarisha, kupeleka na kusambaza maarifa katika sayansi na teknolojia kwa kufundisha, kufanya utafiti na kushauri katika Nyanja mbalimbali nchini.

KIST inatoa elimu ya ufundi kutokana na mabadiliko makubwa ya teknolojia katika dunia ya leo kwenye sekta mbalimbali, kuna kutanuka kwa mianya ya ujuzi wa kiufundi katika soko la ajira la wanayasayansi, mafundi na wahandisi.

www.kist.ac.tz 

 

IOT (Zamani ZITOD)

Ni chuo kinachotoa mafunzo ya kitaaluma na kutoa huduma maalum katika maendeleo makuu ya rasilimali watu kwenye maeneo ya utalii, takrima, ujasiriamali na mawasiliano ya kompyuta. 

 

www.zitod.org

 

ZATI

Ni jumuiya inayoendeshwa na wanachama tokea 2003 ikiwakilisha maslahi  ya wawekezaji katika utalii Zanzibar. Umuhimu wa utalii Zanzibar na athari zake katika uchumi na mchango wa ZATI zinatambulika na serikali.

www.zati.or.tz