Dhana ya kituo cha uwalimu wa mafunzo ya amali ilitengenezwa kuhakikisha muundo, udhibiti wa sifa, na kiwango cha ubora ulioidhinishwa kwa walimu wa Zanzibar. Walimu wapatao 12 wamehitimu mafunzo ya amali kwa Kituo cha mafunzo ya walimu kwani walimu hawa watatoa mafunzo kwa walimu wengine wa vituo vya mafunzo vya amali vya binafsi na Serikali.