50620480 2402469033157423 8711750447313977344 o

Kituo cha mafunzo ya walimu kimesanifiwa kwa ajili ya walimu wa vituo vya mafunzo ya amali ambavyo vitatoa elimu ya lazima ya ufundishaji kwa walimu wa mafunzo ya amali katika njia ya kozi fupi fupi. Kozi hizi zinahakikisha kiwango na sifa za ufundishaji kwa walimu wa Zanzibar. Kituo hichi kitazingatia walimu wa taaluma mbali mbali kutoka vyuo vya mafunzo ya amali vya Serikali na vyuo vya mafunzo ya amali vya binafsi vilivyosajiliwa na MMA.

Kituo cha mafunzo ya walimu pia kitatoa kozi maalum za mafunzo ya amali kwa walimu na wafanyakazi wenye ujuzi katika fani maalum Zanzibar.

Kituo hicho kitapatikana Mkokotoni kwenye eneo la kituo cha mafunzo ya amali.