50620480 2402469033157423 8711750447313977344 o

Sekta ya kibinafsi ndio kiungo muhimu cha maendeleo ya mafunzo ya amali na inahitaji kuchukua jukumu zaidi katika kukuza mafunzo ya amali. Mradi huu utaendelea kufanya kazi kwa karibu ili kurasimisha na kuweka mfumo bora  wa kushirikiana na sekta binafsi Zanzibar. Katika kuboresha maendeleo ya mfumo wa mafunzo ya amali, kutakuwa na shughuli zaidi za kushirikiana na sekta binafsi, kupokea ushauri kutoka makampuni kwa vyuo, kutembelea kampuni, vikao vya umma na mazungumzo, maarifa ya ufundi kubadilishana na kadhalika.