50620480 2402469033157423 8711750447313977344 o

Mfumo ya Dual apprenticeship ni njia inayoongoza na kutambulika kimataifa kwa mafunzo ya amali. Huu ni mfumo wa kuchanganya mafunzo katika vituo vya mafunzo ya amali na kufanya kazi katika sekta binafsi kwa vipindi vinavyowekwa ili kuboresha mbinu na mafunzo zaidi. Matokeo ya mfumo huu kwa wanafunzi, utendaji wa vituo vya mafunzo na uelewa wa sekta binafsi ni mkubwa. Mfumo huu utaweka vigezo vya mpango wa kwanza wa majaribio kwa Zanzibar na utahusisha kwa karibu wadau na washirika wote wanaohusika.